Loading...

Singida United, Yanga waingia vitani

KIPA wa African Lyon, Youthe Rostand ambaye pia anawindwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ni mmoja wa magolikipa wanaowaniwa na timu mpya ya Singida United ambayo msimu ujao itashiriki ligi hiyo, imefahamika.

Makipa wengine ni pamoja na Beno Kakolanya wa Yanga na Said Kipao wa JKT Ruvu ya Mlandizi, Pwani.

Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrahman Sima, alisema ni kweli makipa hao wako katika 'rada' yao na tayari wameshawasilisha kwenye Kamati ya Usajili ya klabu hiyo iliyoko chini ya Waziri wa Mambo Ndani, Mwigulu Nchemba.

Sima aliongeza kuwa jukumu lao ni kuwasilisha kwenye kamati hiyo, lakini mwenye uamuzi wa mwisho ni Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, ambaye kwa sasa ameenda likizo Ghana.

"Ni kweli tumeshaanza mazungumzo ya awali na makipa watatu, lakini nani atapewa mkataba wa kuitumikia timu yetu, tunasubiri uamuzi wa kocha mkuu, hilo suala la kiufundi liko chini yake," alisema Sima.

Aliongeza kuwa wachezaji wote wanaosajiliwa kwenye kikosi cha timu hiyo wanatokana na kupata baraka za Pluijm na hiyo ni kulipa nafasi benchi la ufundi kusajili nyota watakaoisaidia Singida United kushindana na si kusindikiza klabu nyingine katika msimu ujao.

Mbali na Singida United, timu nyingine zilizopanda daraja ni pamoja na Njombe Mji ya Njombe na Lupili FC ya Iringa.
Singida United, Yanga waingia vitani Singida United, Yanga waingia vitani Reviewed by Zero Degree on 4/02/2017 10:18:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.