Loading...

Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya mchezo wa Scrabble

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya mchezo wa Scrabble (pichani) yanayotarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Aprili 14 hadi 16,2017 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa mashindano ya Scrabble, Nicholas Mbugua amesema mashindano hayo yatashirikisha wachezaji 80 kutoka Kenya, Uganda, na Afrika Kusini.

Katika hatua nyingine, Chama cha Wachezaji Scrabble nchini (TASPA) kimeahidi kuufufua mchezo huo hasa katika vyuo vikuu na shule za msingi na sekondari.

Katibu wa TASPA, Toyo Kitua wakati akizungumza na waandishi wa habari, Aprili 10,2017 jijini Dar es Salaam amesema awali walijaribu kuufufua mchezo huo ila walikwama kutokana na ukosefu wa fedha.

“Mara ya kwanza tuliuanzisha lakini tulikwama sababu ya ukosefu wa fedha ila hivi sasa tunataka kuufufua hasa kwenye shule na vyuo nchini. Mchezo huu ni mzuri kwa wanafunzi sababu ni mgumu unaohitaji kutumia akili,” amesema.
Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya mchezo wa Scrabble Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya mchezo wa Scrabble Reviewed by Zero Degree on 4/11/2017 01:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.