Loading...

VIDEO: Je, huu ndio mwisho wa Rodriguez katika klabu ya Madrid?? Kamera zamnasa akimtusi Zidane

Nyota wa Real Madrid, James Rodriguez alimtusi Zinedine Zidane kwa kuita 'mother*****' kwa mfululizo wakati Real ikiibuka na ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Leganes Jumatano.

Raia huyo wa Columbia alianzishwa katika kikosi cha kwanza, ikiwa ni mechi yake ya 8 kwenye La Liga kwa msimu, lakini alitolewa baada ya dakika 72.

Na alipokuwa anatembea kuelekea nje ya uwanja, kamera za televisheni zilichukua kipande kifupi kikimuonyesha nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 akitamka matusi kwa hasira dhidi ya bosi wake huyo wa Madrid.


Kwa mujibu wa Deportes Cuatro, Rodriguez alipokuwa anatembea kuelekea nje ya uwanja alitamka haya: 'Motherf **** r! Kamwe hujawahi kunipa mchezo kamili hata siku moja! '

Rodriguez kisha aliupiga kwa ngumi ukuta uliopo pembeni mwa benchi la wachezaji kabla ya kukaa chini kwenye benchi hilo.

Amekua akihusishwa
 na kuihama Bernabau hivi karibuni, kujiunga na Liverpool, Chelsea pamoja na Manchester United kwa kuwa timu zote hizo zilikua zikionyesha nia ya kumsajili nyota huyo.

Swali ni kwamba: Je, huu ndi mwisho wa James kuitumikia Real Madrid?


VIDEO: Je, huu ndio mwisho wa Rodriguez katika klabu ya Madrid?? Kamera zamnasa akimtusi Zidane VIDEO: Je, huu ndio mwisho wa Rodriguez katika klabu ya Madrid?? Kamera zamnasa akimtusi Zidane Reviewed by Zero Degree on 4/07/2017 04:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.