Habari njema kwa Yanga kuhusu Tambwe na Donald Ngoma kuelekea mechi dhidi ya MC Alger
Yanga huenda ikapata huduma ya washambuliaji wake Donald Ngoma na Amis Tambwe katika mchezo wa kimataifa wa kombe la shirikisho Afrika siku ya Jumamosi dhidi ya MC Alger.
Tambwe na Ngoma ambao wamekosa michezo kadhaa ya Yanga kutokana na majeruhi, kwa sasa wameanza mazoezi ya pamoja na kikosi kizima na wanaendelea vyema kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo Edward Bavu.
Bavu amesema Zulu hakupata athari zozote kwenye mfupa, jeraha lilikuwa kwenye nyama na baada ya siku tano au saba tangu aliposhonwa, watamfanyia uchunguzi kuona kama anaweza kuanza kufanya mazoezi mepesi.
“Ngoma alikuwa majeruhi kwa muda mrefu lakini yupo kwenye kikosi ameshaanza mazoezi karibu siku tano sasa, Amis Tambwe vilevile yupo kwenye mazoezi ikiwa ni siku ya tatu,” amesema Bavu wakati akizungumza na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’.
“Kwa sababu mechi bado haijafika, inawezekana wakawepo katika kikosi kwa hiyo tunabaki na majeruhi wawili Thabani Kamusoko kama mnavyojua yeye aliumia kifundo cha mguu kwenye mazoezi siku moja kabla ya mechi Azam. Anaendelea kupata matibabu na anaendelea vizuri, bado mapema sana kusema ni siku gani ataanza mazoezi. Justine Zulu yeye alipata matatizo kwenye mechi dhidi ya Azam.”
“Zulu alishonwa nyuzi kama sita hivi, kidonda cha kushonwa kinachukua siku si chini ya tano kwa hiyo bado mapema kwa vyovyote mechi ijayo hawezi kucheza labda tutaangalia mechi ya marudiano anaweza kucheza baada ya kumfanyia uchunguzi.”
Bavu amesema Zulu hakupata athari zozote kwenye mfupa, jeraha lilikuwa kwenye nyama na baada ya siku tano au saba tangu aliposhonwa, watamfanyia uchunguzi kuona kama anaweza kuanza kufanya mazoezi mepesi.
Habari njema kwa Yanga kuhusu Tambwe na Donald Ngoma kuelekea mechi dhidi ya MC Alger
Reviewed by Zero Degree
on
4/07/2017 04:12:00 PM
Rating: