Loading...

VIDEO: Samatta alivyoanza mechi za Ligi Kuu ya Ubelgiji kwa kuchungulia nyavu

Ligi Kuu Ubelgiji iliendelea tena jana Jumamosi ya April 1, 2017 kwa KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta kuikaribisha Lokeren katika mchezo wao wa kwanza wa play offs wa Kundi B wa Ligi Kuu Ubelgiji.

Mbwana Samatta ambaye alikuwa katika kikosi cha kwanza cha KRC Genk kilichocheza dhidi ya Lokeren alifanikiwa kuisaidia timu yake ya KRC Genk kupata ushindi wa goli 4-0, Mbwana Samatta akifunga goli la pili dakika ya 72.

Goli la kwanza la Genk lilifungwa na Pozuelo dakika ya 45, goli la tatu lilifungwa na Boetius dakika ya 77 la mwisho lilifungwa na Jose Naranjo aliyeingia dakika ya 84 akitokea benchi na kufunga goli dakika ya 90, ushindi huo umeifanya KRC Genk kuongoza Kundi B lenye timu sita kwa kuwa na magoli mengi.


VIDEO: Samatta alivyoanza mechi za Ligi Kuu ya Ubelgiji kwa kuchungulia nyavu VIDEO: Samatta alivyoanza mechi za Ligi Kuu ya Ubelgiji kwa kuchungulia nyavu Reviewed by Zero Degree on 4/02/2017 02:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.