Wauguzi 11 watiwa mbaroni kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma mkoani Shinyanga.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Muliro Jumanne Muliro |
Wauguzi hao wamebainika kufanya ubadhilifu baada ya mkuu wa wilaya ya Kahama Bw.Fadhili Nkurlu kufanya ziara ya kushtukizia katika hospitali hiyo na kuhoji kushuka kwa mapato katika hospitali hiyo ambapo alilazimika kumuagiza mkaguzi wa ndani wa halmashauri hiyo kufanya ukaguzi katika majalada ya mapato hatua ambayo iliwabainisha watumishi 12 kuhusika na ubadhirifu wa makusanyo ya fedha na mmoja kati yao hajakamatwa kwa madai ya kuwa yuko likizo.
Akithibitisha kwa njia ya simu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Muliro Jumanne Muliro amekiri kukamatwa kwa watimishi hao na kudai kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma hiyo na watakaothibitika watafikishwa mahakamani huku kaimu mkirugenzi wa halmashauri ya Kahama mji Bw.Deogratius Kapami akidai kuwa zoezi hilo limeanza katika hiospitali ya wilaya na linaendelea katika vituo na zahanati zotoe za wilaya ya Kahama.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa mji wa Kahama wameonyesha faraja yao kwa hatua iliyochukuliwa na mkuu wa wilaya huku wakimuomba aingie katika taasisi zingine kuchunguza bado kuna ubadhirifu mkubwa unaofanyika hali itakayonusuru mapato ya serikali na kurejesha huduma bora kwa wananchi.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa mji wa Kahama wameonyesha faraja yao kwa hatua iliyochukuliwa na mkuu wa wilaya huku wakimuomba aingie katika taasisi zingine kuchunguza bado kuna ubadhirifu mkubwa unaofanyika hali itakayonusuru mapato ya serikali na kurejesha huduma bora kwa wananchi.
Wauguzi 11 watiwa mbaroni kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma mkoani Shinyanga.
Reviewed by Zero Degree
on
4/13/2017 02:52:00 PM
Rating: