Waziri mkuu amemsimamisha kazi Mkurugenzi msaidizi wa Pembejeo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi wa Pembejeo, Shenal Nyoni ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kwa kuongeza gharama za pembejeo kwa kushirikiana na baadhi ya mawakala wa pembejeo za kilimo.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo katika kikao alichokiitisha kwenye makazi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma kati yake na mawakala wa pembejeo za kilimo pamoja na maofisa kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Waziri Mkuu aliongeza mawakala wa pembejeo waliwasilisha serikalini deni la Sh bilioni 65.4 kwa huduma waliyoitoa katika mikoa 25 ambapo Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imekamilisha uhakiki wa madeni hayo kwa mikoa 10 ya Morogoro, Iringa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha.
Shenal Nyoni |
Aidha, amesema serikali italipa madeni yote ya mawakala wa pembejeo za kilimo mara baada ya kukamilisha uhakiki na kujiridhisha juu ya uhalali wake, sababu bado inawahitaji mawakala ili kushirikiana nao katika kuhudumia wakulima kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo katika kikao alichokiitisha kwenye makazi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma kati yake na mawakala wa pembejeo za kilimo pamoja na maofisa kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Waziri Mkuu aliongeza mawakala wa pembejeo waliwasilisha serikalini deni la Sh bilioni 65.4 kwa huduma waliyoitoa katika mikoa 25 ambapo Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imekamilisha uhakiki wa madeni hayo kwa mikoa 10 ya Morogoro, Iringa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha.
Waziri mkuu amemsimamisha kazi Mkurugenzi msaidizi wa Pembejeo
Reviewed by Zero Degree
on
4/11/2017 02:55:00 PM
Rating: