Loading...

Andrew Vincent ‘Dante’ alikua na haya ya kusema kwa wanaomtukana kisa kujifunga

BEKI wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ amewajibu wanaomkosoa kutokana na kujifunga kwake kwa kuwaambia kwamba hawajui soka.

Dante amejibu shutuma hizo baada ya Jumapili kujifunga bao katika mchezo wa nusu fainali ya kombe Azam Sports Federation dhidi ya Mbao na kuondoshwa kwenye mashindano baada ya kufungwa bao 1-0.

‘Dante’ amesema: “Mpira ni mchezo wa makosa lakini wapo watu wanaongea sana maneno mabaya kuhusu tukio la kujifunga lakini kwa upande wangu dhamira yangu ilikuwa kuokoa na siyo kufunga.”

“Inaniuma lakini ndiyo imeshatokea kwenye maisha utakutana na kila kitu kama vile kizuri au kibaya, kwahiyo kwangu mimi nawaacha waongee mpaka basi ila mimi najua ni bahati mbaya,” amesema Dante.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amesema wamekosa kombe la shirikisho (FA) kwahiyo malengo yao kwa sasa ni kukaza kwenye ligi kuu huku akiwa na uhakika wa kushinda viporo vyao viwili vilivyobaki.
Andrew Vincent ‘Dante’ alikua na haya ya kusema kwa wanaomtukana kisa kujifunga Andrew Vincent ‘Dante’ alikua na haya ya kusema kwa wanaomtukana kisa kujifunga Reviewed by Zero Degree on 5/03/2017 02:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.