Loading...

Tuchel amzodoa Ashley Young


Meneja wa PSG Thomas Tuchel amemkosoa beki wa Manchester United Ashley Young kwa kumpiga kikumbo Angel di Maria katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Jumanne katika dimba la Old Trafford. Kitendo cha Young kumpiga kikumbo Di Maria kiliwakera nyota wa PSG. Hata hivyi, hakuonyeshwa kadi yoyote.

Tuchel aliamini kuwa hakukuwa na sababu yoyote ya kufanya vile na Young alistahiri kupewa kadi. Mjerumani huyo alisema, “Nafikiri alikuwa na bahati kwani hakukuwa na sababu yoyote ya kufanya vile – amecheza sana katika dimba hili na anaelewa kuwa kuna mteremko kidogo kuelekea chini. Hakukuwa na ulazima wa kumsukuma Di Maria kwenye wigo. Sijui kama ilikuwa makusudi na nafuraha kwa sababu hakuumia.”

Angel di Maria alirejea Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu aondoke Manchester United. Mashabiki wa Manchester United walikuwa wakimzomea katika mchezo wote. Hata hivyo, Di Maria ndiye aliyeondoka uwanjani akichekelea kwa kutoa 'assist' ya magoli yote ya PSG.

Tuchel alisifia kiwango cha Di Maria, akisema, “Di Maria ni mchezaji mwenye ushindani. Kama utamcheka, haitamfanya kuwa dhaifu. Nilifikiri alikuwa na uhusiano mzuri na mashabiki. Alikuwa na wasiwasi na alihitaji kutulizi akili kidogo katika kipindi cha kwanza. Mwishoni alifanya vizuri sana.”

Kwa magoli mawili ya ugenini, PSG wana nafasi kubwa ya kusonga hatua ya robo fainali kuelekea mchezo wao wa marudio wiki mbili zijazo. Kabla ya hiyo, wana michezo mitano. Wa kwanza ukiwa ni dhidi ya Saint-Etienne kwenye 
Ligue 1 Jumapili.
Tuchel amzodoa Ashley Young Tuchel amzodoa Ashley Young Reviewed by Zero Degree on 2/16/2019 07:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.