Aveva kulipeleka sakata la pointi 3 za Kagera Sugar mbele ya Shirikisho la soka duniani [FIFA]
Baada ya Kamati ya maadili na hadhi za wachezaji kuipoka klabu ya Simba SC alama tatu ilizopewa na kamati ya saa 72, rais wa klabu ya hiyo, Evans Aveva amezungumza na waandishi wa habari hii leo na kuelezea maamuzi ya klabu hiyo.
Kamati hiyo ilitengua uamuzi wa awali uliofanywa na kamati ya saa 72 ulioipa Simba pointi tatu baada ya kubaini Mohammed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano kabla ya mchezo wa Simba na Kagera uliochezwa Aprili 2 mkoani Kagera.
Rais wa Simba, Evance Aveva amewaambia wanahabari leo katika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi kuwa wanangojea barua kutoka bodi ya ligi kabla ya kwenda Fifa.
Swala lingine ambalo Rais Aveva amelizungumzia ni juu ya mchezo wao wa fainali kati ya Simba Sc dhidi ya klabu ya Mbao Fc, na kusema kuwa wanaomba waendeshaji wa mashindano hayo pamoja na wadhamini wake kupewa heshima inayoambatana na mashindano kwa kuwa ni makubwa na yanatoa mshiriki wa kimataifa na hivyo kuna umuhimu wa kutoa ratiba ya mapema na sio kuchelewa kutoa ratiba ya Viwanja.
Aveva amesema Simba SC wanaonewa katika hilo na kamwe hawawezi kulikalia kimya swala hilo, na kwa sasa wanangoja barua ya maandishi kutoka kwenye bodi ya shirikiso la soka nchini, TFF, ili kulipeleka swala hilo kwenye shirikisho la soka duniani, FIFA pamoja na kulipeleka suala hilo katika mahakama ya michezo CAS.
Kuhusiana na maamuzi hayo yaliyotolewa na TFF kupitia kwa katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa, TFF walishasema Simba haiwezi kukata rufaa tena.
Wao kama Simba Sc wanaona alama tatu ni mali yao, na hivyo kuna mkanganyiko kati ya Bodi na kamati ya haki na hadhi za wachezaji, na kwao wanajua kadi tatu zilikuwepo kwa kuwa hakuna kamati hata moja inayopinga suala hilo.

Aveva, amesema watapeleka malalamiko yao katika Shirikisho la soka duniani (FIFA) juu ya kupokonywa alama tatu za mezani walizopata baada ya Kagera Sugar kumchezaji mchezaji mwenye kadi tatu za njano.
Kamati hiyo ilitengua uamuzi wa awali uliofanywa na kamati ya saa 72 ulioipa Simba pointi tatu baada ya kubaini Mohammed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano kabla ya mchezo wa Simba na Kagera uliochezwa Aprili 2 mkoani Kagera.
Rais wa Simba, Evance Aveva amewaambia wanahabari leo katika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi kuwa wanangojea barua kutoka bodi ya ligi kabla ya kwenda Fifa.
“Nawaomba wanachama na mashabiki watulie. Pointi tatu ni mali ya Simba, hadi sasa kamati iliyotengua uamuzi wa awali haikuwa na mamlaka hayo. Tunakwenda Fifa kudai haki yetu.
“Hatuwezi kurudi tena kamati ya saa 72, tuna mashauri yetu mengi lakini hayasikilizwi na kutolewa uamuzi ni bora twende ngazi za juu,”amesema Aveva.
Swala lingine ambalo Rais Aveva amelizungumzia ni juu ya mchezo wao wa fainali kati ya Simba Sc dhidi ya klabu ya Mbao Fc, na kusema kuwa wanaomba waendeshaji wa mashindano hayo pamoja na wadhamini wake kupewa heshima inayoambatana na mashindano kwa kuwa ni makubwa na yanatoa mshiriki wa kimataifa na hivyo kuna umuhimu wa kutoa ratiba ya mapema na sio kuchelewa kutoa ratiba ya Viwanja.
Amesema hawana tatizo na Dodoma na watatangulia huko mapema kwani wanaiheshimu sana Mbao Fc ila kamwe hawaiogopi na wapo tayari kucheza hata wangepangiwa kiwanja chochote.
Aveva kulipeleka sakata la pointi 3 za Kagera Sugar mbele ya Shirikisho la soka duniani [FIFA]
Reviewed by Zero Degree
on
5/04/2017 12:21:00 AM
Rating: