Beki wa Serengeti boys apata shavu Hispania
BEKI wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Dickson Job, yupo mbioni kujiunga na moja ya vituo vya kukuza vipaji ‘academy’ iliyopo nchini Italia au Hispania.
Dickson Job |
Taarifa zinasema kwamba, meneja wa mchezaji huyo chipukizi yupo kwenye mazungumzo na wakala raia wa Cameroon, Olivier Noah, anayetambulika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Alisema Job atajiunga na moja ya academy za nchini humo na akifikisha miaka 18 ataingia mkataba wa kuichezea timu kubwa huko huko.
Job alipewa kitambaa cha unahodha wa Serengeti Boys katika michuano ya Kombe la Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 inayoendelea nchini Gabon, baada ya kuumia Issa Abdi Makamba.
“Olivier ni Mcameroon anayefanya shughuli zake za uwakala barani Ulaya na tupo naye kwenye mazungumzo kuona ni namna gani Job ataenda kujiunga na ‘academy’ ya Italia au Hispania,” alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Alisema Job atajiunga na moja ya academy za nchini humo na akifikisha miaka 18 ataingia mkataba wa kuichezea timu kubwa huko huko.
Job alipewa kitambaa cha unahodha wa Serengeti Boys katika michuano ya Kombe la Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 inayoendelea nchini Gabon, baada ya kuumia Issa Abdi Makamba.
Beki wa Serengeti boys apata shavu Hispania
Reviewed by Zero Degree
on
5/24/2017 02:46:00 PM
Rating: