Loading...

Conte amemtaja mchezaji anayefaa kumrithi Terry kwenye nafasi ya Unahodha msimu ujao

Ligi kuu ya Uingereza kwa msimu huu imefika mwisho na wengi wanajaribu kujiuliza ni nani atakaye kuwa Nahodha wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza 2016/17 kwa msimu ujao!

Kufuatia kuondoka kwa nahodha wa sasa, John Terry, mashabiki wanahamu ya kusikia ni nani atayekuwa mrithi wake kwa msimu ujao ambapo Chelsea pia itashiriki Ligi ya Mabingwa (UEFA). 

Kwa kushiriki katika michezo 700 kwa timu yake, kuisaidia timu yake kubeba Mataji 6 ya Ligi Kuu ya Uingereza, mataji 6 ya FA Cup, na Taji 1 la Ligi ya mabingwa (UEFA) akishirikiana na wachezaji wenzake katika nyakati tofauti, itakua ni ngumu kidogo kumpata mrithi wa Terry.


Garry Cahill amekua akibeba jukumu la Unahodha wakati Terry alipokua katika Benchi, hata hivyo, Garry Cahill ndiye atakayekuwa Nahodha mpya wa Chelsea msimu ujao?

Hata hivyo, mwamuzi wa mwisho katika hilo ni meneja wa chelsea, Antonio Conte ambaye aliulizwa juu ya jambo hilo na waandishi wa habari.
"Garry amekuwa Nahodha msaidizi msimu huu. Ametekeleza majukumu ya unahodha wakati ambapo John Terry hakucheza", alisema Conte.

“Kwa hakika, Garry ana sifa kubwa ya kuwa Nahodha, lakini kwa sasa ni vema kufikiria zaidi kuhusu kumalizia msimu huu.

“kuanza kufikiria kuhusu msimu ujao ni hatari sana kwa sababu bado tuna malengo mengine tunahitaji kuyafikia kabla ya msimu kuisha.”
Conte amemtaja mchezaji anayefaa kumrithi Terry kwenye nafasi ya Unahodha msimu ujao Conte amemtaja mchezaji anayefaa kumrithi Terry kwenye nafasi ya Unahodha msimu ujao Reviewed by Zero Degree on 5/20/2017 08:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.