Loading...

Hii ndio GR5, ...ni Simu mpya iloyozinduliwa na Kampuni ya Huawei

Kampuni ya simu ya Huawei Tanzania imeingiza sokoni simu za kisasa yenye kamera mbili zenye ubora wa hali ya juu inayoitwa GR5 2017 huku ikifanya juhudi kuboresha biashara yake kwenye soko la ndani la Tanzania kwa mwaka huu. Kulingana na takwimu za robo ya kwanza ya mwaka 2016, Kampuni ya Huawei Tanzania inashikilia nafasi ya pili huku ikiwa na umiliki wa soko wa asilimia 22 unaoendelea kuongezeka sambamba na soko la Tanzania la simu linalokua kwa kasi.

GR5 2017 ni simu ya kwanza kabisa katika soko la ndani la simu za aina ya smartphone yenye kamera mbili zenye nguvu katika orodha ya simu za kiwango cha kati. Simu hii yenye kamera mbili ina RAM ya 3GB, Diski Uhifadhi ya 32GB, betri linalohifadhi chaji kwa muda mrefu, teknolojia ya alama za vidole ya 3.0 na kioo cha FHD chenye inchi 5.5.

Akizungumza kuhusiana na simu hii mpya sokoni, Mkurugenzi wa kanda wa Kampuni ya Huawei, Ndugu Mark Ho alisema licha ya kuwepo ushindani mkali, biashara ya kampuni ya simu za smartphone inaendelea kukua kwenye soko la ndani. Alihusisha ukuaji wa kampuni na mkakati wa kumgusa zaidi mteja unaolenga kuunda uvumbuzi wa maana, pamoja na dhamira endelevu ya kutengeneza chapa ya kisasa na kuboresha vituo vya mauzo rejareja na uwezo wa huduma baada ya mauzo.

Simu ya GR5 2017 imetengenezwa kwa ajili ya wapenda teknolojia wanaotafuta simu ya kisasa ya bei nafuu. Kama ilivyo kwa mtangulizi wake – Huawei GR5, simu ya Huawei GR5 2017 ina vipengele na teknolojia inayozidi hata zile simu za bei ghali sana. Ina ufanisi wa hali ya juu, betri la kipekee inayotumia teknolojia ya kutunza umeme ambayo inakuhakikishia matumizi ya chaji moja kwa kipindi cha siku moja na nusu kwa matumizi ya kawaida.

“Katika mwaka huu, ili tuweze kudumisha ukuaji endelevu sio tu wa kitaifa bali na kimataifa pia, tunapanga kuboresha minyororo yetu ya usambazaji, vituo vyetu, huduma na maeneo mengine mbalimbali yatakayotusaidia kurahisisha shughuli zetu, kuboresha ufanisi wetu na utekelezaji, kusukuma mkakati wetu wa kusambaa kimataifa zaidi na kuendeleza kwa vitendo uwezo wetu wa hapo baadae,” alisema Ndugu Mark Ho.

“Simu ya Huawei GR5 2017 inazingatia hitaji kubwa la wateja wa simu za smartphone ambazo ni bora na za bei nafuu zenye ufanisi mkubwa, burudani na uzoefu mzuri wa upigaji picha,” alisisitiza Ndugu Mark Ho. Simu hii inakuja baada ya mafaniko makubwa ya simu zenye teknolojia ya hali ya juu ikiwa ni pamoja na Mate 8, Mate 7, Mate S, P9, P9 lite, P8, P8 lite, Y3 lite,Y3 II, Y3 C, ili kuhakikisha wateja wa Tanzania wanakuwa na wigo mpana wa vifaa za Huawei vya bei nafuu, ambavyo vinakidhi mahitaji ya wateja wa vipato tofauti tofauti na mtindo unaotofautiana wa maisha.

Kampuni ya Huawei inaendelea kuyapa kipaumbele mahitaji ya wateja na kuboresha uwezo wake wa kuwafikia wateja katika vituo vyake, uuzaji wa moja kwa moja, chapa, masoko na huduma. Hivyo, inaboresha wigo wa biashara zake na kuhuisha shughuli zake na huduma kwa wateja. Simu ya GR5 2017 itakuwa ikiuzwa nchini kwa bei ya reja reja ya TZS 685,000/= na inapatikana katika rangi ya kijivu, dhahabu na fedha.

Kampuni ya Huawei pia imejiimarisha kuendeleza uwepo wake kwenye soko la simu za smartphone, vifaa vya nyumbani na huduma ya kuhifadhi taarifa kwenye ‘cloud’, ikiwa na lengo la kuwa mtoa huduma wa jukwaa na utoaji suluhisho la mwanzo hadi mwisho, huku ikiwapa wateja njia rahisi na bora ya kuyaunganisha maisha yao. Inaendelea kujijenga kupitia uwezo wake mkubwa ili kuwa kiongozi hapo baadae na kuwa chapa maarufu na kwa wateja.
Hii ndio GR5, ...ni Simu mpya iloyozinduliwa na Kampuni ya Huawei Hii ndio GR5, ...ni Simu mpya iloyozinduliwa na Kampuni ya Huawei Reviewed by Zero Degree on 5/18/2017 01:04:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.