Loading...

Hii ndio rekodi iliyovunjwa na Harry Kane Tottenham 'North London Derby'

STRAIKA Harry Kane amevunja rekodi baada ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Tottenham kufunga mabao mengi katika ‘derby’ za Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal, wakati juzi alipocheka na nyavu kwa njia ya penalti katika mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa White Hart Lane.

Kabla ya mchezo huo, Kane alikuwa akifukuzia kufikisha mechi ya nne, akifunga mabao katika mechi hiyo na huku Tottenham wakiwa na dhamira ya kuendelea kuifukuza Chelsea katika mbio za kuwania ubingwa.

Alikuwa ni straika Dele Alli aliyeipatia Spurs bao la kuongoza dakika ya 55 na dakika mbili baadaye, baada ya Gabriel kumwangusha Kane ndani ya eneo la hatari, staa huyo wa timu ya Taifa ya England akapata nafasi ya kuongeza rekodi yake dhidi ya Arsenal.

Baada ya kupata penalti hiyo, Kane hakufanya makosa kwa kumchambua mlinda mlango Petr Cech na hivyo kufikisha bao lake la 21 katika michuano ya Ligi Kuu msimu huu.

Kwa kufunga bao hilo, ina maana kwamba Kane atakuwa ameifungia Tottenham mabao sita dhidi ya Arsenal, likiwa ni moja zaidi dhidi ya mchezaji yeyote ambaye amewahi kucheza mechi zilizowakutanisha miamba hao.
Hii ndio rekodi iliyovunjwa na Harry Kane Tottenham 'North London Derby' Hii ndio rekodi iliyovunjwa na Harry Kane Tottenham 'North London Derby' Reviewed by Zero Degree on 5/02/2017 05:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.