Loading...

NEC imetangaza nafasi ya Ubunge Viti maalumu Chadema

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi ya mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya Chadema.

Nafasi hiyo imetangazwa baada ya kifo mbunge aliyekuwa anashikilia wadhfa huo, Dk Elly Macha kufariki dunia Machi 31, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumanne) na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage ni kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjulisha kuwepo kwa nafasi hiyo.

“Kutokana na kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge wa Viti Maalum, taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia Ibara ya 78 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343,”amesema.
NEC imetangaza nafasi ya Ubunge Viti maalumu Chadema NEC imetangaza nafasi ya Ubunge Viti maalumu Chadema Reviewed by Zero Degree on 5/02/2017 06:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.