Loading...

Hivi ndivyo Vipengele 3 vilivyoongezwa kwenye Tuzo za Ligi Kuu ya Tanzania Bara

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 akimkabidhi tuzo mchezaji wa yanga Abdul Juma,aliyeibuka mchezaji bora wa mwaka wa ligi. Hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Sherehe za Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kufanyika Mei 24 mwaka huu ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam huku vipengele viwili vikiwa vimeongezwa katika tuzo za msimu huu.

Baadhi ya wachezaji walioshinda tuzo za msimu uliopita. Kutoka kushoto ni Ibrahim Ajibu (Goli Bora), Aishi Manula (KIpa Bora), Juma Abdul (Mchezaji Bora), Thaaban Kamusoko (Mchezaji Bora wa nje) na Mohamed Hussein (Mchezaji Bora Chipukizi)
Tuzo zilizoongezwa ni: Tuzo ya Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia nzuri kwa soka la Tanzania).

Nyingine ni: Tuzo ya Kikosi Bora cha Msimu (Itatolewa kwa wachezaji Bora 11 wa Ligi Kuu (VPL XI 2016/2017) walioteuliwa kutokana na ufanisi wao katika ligi hiyo msimu huu.

Pia imeongezwa Tuzo ya Mchezaji Bora mwenye chini ya umri wa miaka 20 (Hii itatolewa kwa wachezaji waliofanya vizuri katika ligi ya vijana ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom.

Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya Vijana itajulikana kama Tuzo ya Ismail Khalfan ikiwa ni heshima ya kumbukumbu ya mchezaji Ismail Khalfan wa Mbao FC aliyefia uwanjani katika mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kagera.

Kutokana na mabadiliko hayo tuzo zitakazotolewa katika sherehe hizo pamoja na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya VPL ambayo ndiyo tuzo kuu, pia ni Bingwa wa Ligi Kuu, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na Mfungaji Bora.

Nyingine ni Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, Golikipa Bora, Kocha Bora, Mwamuzi Bora, Mchezaji Bora wa Heshima, Mchezaji Bora anayechipukia, Goli Bora la Msimu, Mchezaji Bora wa Kigeni, Mchezaji Bora wa Chini ya Umri wa Miaka 20 na Timu Yenye Nidhamu.

Tuzo za Bingwa, mshindi wa pili, wa tatu na wa nne na Mfungaji Bora hizi zipo kulingana na msimamo wa ligi ulivyo.

Hata hivyo Mfungaji Bora safari hii kuna wachezaji wawili wamefungana, hivyo kamati itapitia vigezo vilivyopo katika Kanuni za kumpata Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara ili kupata mshindi ambaye atatangazwa siku hiyo ukumbini.

Wafuatao wameteuliwa kuwania tuzo hizo kutokana na vigezo mbalimbali:
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu
  • Aishi MANULA - Azam
  • Simon MSUVA - Yanga
  • Shiza KICHUYA - Simba
  • Haruna NIYONZIMA - Yanga
  • Mohammed HUSSEIN – Simba
KIPA BORA
  • Aishi MANULA - Azam
  • Owen CHAIMA - Mbeya City
  • Juma KASEJA - Kagera Sugar
  • KOCHA BORA
  • Joseph OMOG - Simba
  • Mecky MEXIME - Kagera Sugar
  • Ettiene NDAYIRAGIJE - Mbao
MWAMUZI BORA
  • Shomari LAWI – Kigoma
  • Elly SASII – Dar es Salaam
  • Hance MABENA - Tanga
  • MCHEZAJI BORA WA KIGENI
  • Haruna NIYONZIMA - Yanga
  • Method MWANJALE - Simba
  • Yusuph NDIKUMANA - Mbao
MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA
  • Mbaraka ABEID - Kagera Sugar
  • Shaaban IDD - Azam
  • Mohammed ISSA - Mtibwa
  • TUZO YA ISMAIL KHALFAN – (U-20)
  • Shaaban IDD - Azam
  • Abdalah MASOUD - Azam
  • Mosses KITAMBI - Simba
TUZO YA HESHIMA
  • (Atatangazwa aliyeteuliwa siku hiyohiyo ya sherehe za tuzo).
GOLI BORA LA MSIMU
  • (Tayari yamepatikana mabao bora 10 ambayo yataoneshwa siku hiyo ukumbini ikiwemo lile bora la msimu mzima).
TIMU YENYE NIDHAMU
  • (Mshindi atatangazwa ukumbini siku hiyo kulingana na vigezo vilivyopo).
WACHEZAJI 11 BORA WA MSIMU – VPL XI 2016/17
  • (Watatangazwa ukumbini siku hiyo ya sherehe).
Hivi ndivyo Vipengele 3 vilivyoongezwa kwenye Tuzo za Ligi Kuu ya Tanzania Bara Hivi ndivyo Vipengele 3 vilivyoongezwa kwenye Tuzo za Ligi Kuu ya Tanzania Bara Reviewed by Zero Degree on 5/22/2017 03:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.