Loading...

Harry Kane ashinda tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uingereza 2016/17

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Kane ameibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya England kwa msimu wa 2016/2017.

Mshambuliaji huyo amemaliza msimu kwa kufunga jumla ya mabao 29 akiwa kacheza kwa dakika 2531, huku akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 87.

Kane anaibuka mfungaji bora kwa msimu wa pili mfululizo msimu uliopita alifunga mabao 25 na kuwa mfungaji bora.Haki miliki ya pichaGOOGLEImage captionRomelu Lukaku amemaliza msimu na mabao 25 goli nne nyumba ya Harry Kane

Wachezaji wanaofuati kwa ufungaji bora ni Romelu Lukaku wa Everton mwenye magoli 25 akifuatiwa na Alexis Sánchez wa Arsenal mwenye mabao 24.

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amemaliza msimu akiwa na magoli 20, nae Sergio Aguero akimaliza na mabao 20.
Harry Kane ashinda tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uingereza 2016/17 Harry Kane ashinda tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uingereza 2016/17 Reviewed by Zero Degree on 5/22/2017 07:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.