Loading...

Huu ndio Mti wa ajabu uliokuwa ukitoa sauti kama binadamu ukipinga kung'olewa jijini Mwanza

Wakazi wa Barabara ya Iloganzala Jijini Mwanza jana walipigwa butwaa baada ya mti kutoa sauti kama binadamu ukipinga using'olewe.




Tukio hilo limetafsiriwa kuwa la kishirikina ama mazingaombwe ikizingatiwa kwamba si jambo lenye uhalisia mti kuongea kama binadamu.

Katika eneo la Iloganzala Jijini Mwanza kuna upanuzi wa barabara inayoelekea Uwanja wa ndege wa Mwanza.

Shughuli ya kuung'oa mti huo aina ya mwembe leo imeendelea ikiwa ni siku ya pili ya kukabiliana na mwembe huo na hatimaye wamefanikiwa kuung'oa huku mamia ya wananchi wakishuhudia tukio hilo la ajabu
Huu ndio Mti wa ajabu uliokuwa ukitoa sauti kama binadamu ukipinga kung'olewa jijini Mwanza Huu ndio Mti wa ajabu uliokuwa ukitoa sauti kama binadamu ukipinga kung'olewa jijini Mwanza Reviewed by Zero Degree on 5/16/2017 11:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.