Loading...

Umeisikia hii ya msichana wa Miaka 10 kuruhusiwa kutoa mimba?

Jopo la madaktari limekubali ombi la msichana wa umri wa miaka 10, ambaye ni muathirika wa matukio yaa ubakaji kutoka jimbo la Haryana kaskazni mwa India la kutoa mimba.

Dr Ashok Chauhan aliiambia BBC kuwa hatua hiyo sasa inaweza kuchukuliwa wakati wowote.

Msichana huyo alipata ujauzito karibu miezi mitano iliyopita. Anadaiwa kubakwa na baba wa kambo ambaye amekamatwa.

Sheria nchini India haziruhusu utoaji mimba baada ya wiki 20, bila ya idhini ya madaktari kuwa maisha ya mwanamke mjamzito yako hatarini.

Uamuzi wa kumruhusu msichana huyo kutoa mimba ulichukuliwa baada ya mahakama kuwaambia madaktari kuwa itakubali.

India ni mojawapo ya mataifa ambayo idadi kubwa ya watoto wanaonyanyaswa kingono.

Hata hivyo uwezekano wa kulizungumzia suala hilo kwa uwazi ni mdogo sana na ni nadra kuzungumziwa hadharani.

Uchunguzi unaonyesha kuwa kesi nyingi kama hii ya mtoto wa miaka kumi, hufatafutiwa ufumbuzi kwa wale wanaofahamika ikiwa ni kwa watoto wenyewe hasusani wanaowalea kama wazazi, jamaa na walimu.
Umeisikia hii ya msichana wa Miaka 10 kuruhusiwa kutoa mimba? Umeisikia hii ya msichana wa Miaka 10 kuruhusiwa kutoa mimba? Reviewed by Zero Degree on 5/16/2017 11:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.