Loading...

Liverpool yakalia nafasi ya 4 na kuifanya Arsenal kuikosa UEFA pamoja na ushindi wa goli 3-1

Arsenal imeshindwa kufuzu kwa kombe la klabu bingwa barani ulaya, Champions League kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20 licha ya ushindi wake dhidi ya Everton wa mabao 3-1 katika siku ya mwisho ya mechi za Primia League.

Arsenal ilianza mechi vizuri ikiwa pointi moja nyuma ya Liverpool na walikuwa katika nafasi bora kuchukua nafasi yao wakati waliongoza mnamo dakika ya nane.

Lakini ukakamavu wa Liverpool uliiwezesha kusalia katika timu nne za kwanza baada ya kuwatandika Middlesbrough mabao 3-0.

Manchester City ilijihakikishia nafasi ya tatu baada ya kuinyuka Watfoird mabao 5-0.
Liverpool yakalia nafasi ya 4 na kuifanya Arsenal kuikosa UEFA pamoja na ushindi wa goli 3-1 Liverpool yakalia nafasi ya 4 na kuifanya Arsenal kuikosa UEFA pamoja na ushindi wa goli 3-1 Reviewed by Zero Degree on 5/21/2017 10:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.