Loading...

Mabosi wa kichina AC Milani wameanza kazi ya kusaka nyota wapya

Nyota huyu amekua akihusishwa na kujiunga na Arsenal. Kwa upande wake mwenyewe amesema klabu anayoipenda ni Manchester United, lakini ni mshabiki mkubwa wa mmchezaji wa zamani wa Chelsea, Michael Essien
na Yaya Toure wa Man City.

Wakati huo huo, na Liverpool, Everton, pamoja na Paris Saint-Germain pia wamekuwa wakiisaka saini ya Franck Kessie.

Badala yake, DiMarzio wanatoa ripoti, inayodai kwamba kinda huyo mwenye miaka 20 toka Ivory Coast yuko katika harakati za kujiunga na klabu ya Serie A, AC Milan ambayo inakumbana na ushindani toka kwa Roma.

Imeripotiwa kwamba, Atalanta watalipwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 31 kama ada ya uhamisho wa Kessie. Kama ni kweli basi kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ivory Coast ana nafasi ya kujifunza mambo mengi kutoka kwa nahodha wa Milan, Riccardo Montolivo.

Kessie amefunga magoli 7 na ametoa 'assist' 4 katika msimu huu. Ameshashiriki mechi 15 za kimataifa akiwa na Ivory Coast.
Mabosi wa kichina AC Milani wameanza kazi ya kusaka nyota wapya Mabosi wa kichina AC Milani wameanza kazi ya kusaka nyota wapya Reviewed by Zero Degree on 5/17/2017 10:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.