Loading...

Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam afariki Dunia

Mwanasiasa mkongwe na Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Kitwana Kondo

Mwanasiasa mkongwe na Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Kitwana Kondo amefariki dunia leo katika Hospitali ya Hindu Mandal,jijini hapa alikokuwa akitibiwa.

Mtoto wa marehemu, Adnan Kondo amethibitisha kifo cha Kondo na kueleza kuwa alifariki saa 10 jioni leo katika hospitali ya Hindu Mandal.

“Kazi ya Mungu haina makosa, ni kweli baba amefariki na siwezi kuzungumza zaidi ya hapo,” amesema Adnan ambaye ni diwani wa kata ya Upanga. Amesema mazishi yatafanyika kesho baada ya swala ya alasiri.
Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam afariki Dunia Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam afariki Dunia Reviewed by Zero Degree on 5/24/2017 10:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.