Loading...

Donald Trump alivyokutana na Papa Francis

Papa Francis akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Marekani, Donald Trump na familia yake akiwepo mke wake Melania Trump na mtoto wake Ivanka Trump.
Rais wa Marekani, Donald Trump amekutana na Papa Francis kwenye makazi yake Vatican, Italia ikiwa ni sehemu ya ziara yake ambayo ameanza kuifanya kwa mara ya kwanza tangu alipoingia madarakani.


Katika ziara hiyo ya Trump nchini Italia, pia atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Italia, Sergio Mattarella na Waziri Mkuu wa Italia, Paolo Gentiloni.

Trump amewasili Italia akitokea Israel ambapo alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu kuhusu uhusiano wa mataifa hayo na jinsi yanavyoweza kuendeleza ushirikiano uliopo baina yao.

Ziara ya Trump ilianzia nchini Saudi Arabia na baada ya hapo akaelekea Israel, sasa Italia na baada ya hapo ataelekea Brussels, Ubelgiji kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO).
Donald Trump alivyokutana na Papa Francis Donald Trump alivyokutana na Papa Francis Reviewed by Zero Degree on 5/24/2017 10:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.