Loading...

Gwajima amewasha moto kwa mara nyingine tena

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
Baada kuwa kimya kwa muda na kuacha kuzungumzia suala la Bashite, Mchungaji wa Kanisa la Ufufu na Uzima, Josephat Gwajima asema, “dude limewashwa” na kwamba anatarajia kuibua suala hilo tena.

Mchungaji huyo ambaye mapema Machi mwaka huu akiwa kwenye mahubiri kanisani kwake, alidai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatumia cheti cha kidato cha nne chenye jina la Daudi Albert Bushite.

Gwajima ambaye alitajwa kwenye orodha ya Makonda kuhusu sakata la dawa za kulevya, amesema atafufua aliyoyasema Makonda ‘Bashite’ wakati wa mahojiano kati yake na kituo cha televisheni cha Star tv yaliyofanywa Jumatatu.

Gwajima amesema, “ Dude limewashwa, nifafanua aliyoyasema Bashite, nitaelezea uraia na mmiliki wa kituo cha tv alichokitumia Jumatatu, nitaeleza ukwepaji kodi wake na vyeti vya watangazaji wake na mishahara yao.”
Gwajima amewasha moto kwa mara nyingine tena Gwajima amewasha moto kwa mara nyingine tena Reviewed by Zero Degree on 5/24/2017 07:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.