Loading...

SportPesa wamezindua Ligi ya Tanzania na Kenya "SportPesa Super Cup", Ratiba kamili ipo hapa

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa leo imezindua ligi itakayojulikana kama SportPesa Super Cup.

Ligi hiyo itashirikisha timu nne kutoka Tanzania na Kenya ambayo itachezwa kutafuta bingwa na mshindi wa pili.

Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema ligi hiyo inatarajiwa kuanza Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11.

“Utakuwa ni ushindani wa timu nne, kutoka Tanzania na Kenya. Hawa ni majirani na siku zote ni wapinzani wakubwa,” alisema.

Bingwa wa SportPesa Super Cup ataondoka na kitita cha dola 30,000 huku mshindi wa pili akipata dola 10,000.

SportPesa ndiyo wadhamini wapya wa timu tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni rekodi mpya.

Tayari wameidhamini Simba kwa mkataba wa miaka mitano, halafu wakafanya hivyo kwa wakongwe wengine Yanga kabla ya kuidhamini Singida United ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu.

Sport Pesa Super Cup:
  • 5/6 Singida united Vs FC leopard
  • Yanga Vs Tusker fc
  • 6/5 Simba Vs Nakuru All Star
  • Jang`ombe boys vs Gor mahia
Nusu fainali tarehe 8

Bingwa wa mechi kati ya Singida united vs AFC leopard atacheza na bingwa kati ya Yanga na Tusker.

Nusu fainali ya pili Bingwa wa mechi kati ya Simba na Nakuru all star atacheza na bingwa wa mechi kati ya Jangombe boyz na Gor mahia.

Ligi itashirikisha timu za Kenya na Tanzania na ligi itashirikisha timu nane na mshindi atapata dola 30,000 sawa na milioni 60 na mshindi wa pili dola 10,000.
SportPesa wamezindua Ligi ya Tanzania na Kenya "SportPesa Super Cup", Ratiba kamili ipo hapa SportPesa wamezindua Ligi ya Tanzania na Kenya "SportPesa Super Cup", Ratiba kamili ipo hapa Reviewed by Zero Degree on 5/24/2017 06:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.