Loading...

Mkongwe mwenye rekodi ya kufunga 'Hat-Trick' ya kasi katika soka afariki

Mchezaji aliyefunga 'hat-trick' (kufunga mabao matatu mechi moja) ya kasi zaidi katika soka, Tommy Ross, amefariki dunia akiwa na miaka 71.

Ross aliweka rekodi ya dunia inayotambuliwa na Guinness World Record kwa kufunga mabao matatu katika muda wa sekunde 90 akiwa na miaka 18.

Wakati huo alikuwa anachezea Ross County dhidi ya Nairn County mwaka 1964.

Rekodi ya awali ilikuwa imewekwa na mchezaji wa Gillingham miaka ya 1950.

Ross baadaye alichezea klabu nyingine za England zikiwemo Peterborough United, Wigan Athletic na York City, pamoja na Brora Rangers ya Scotland.

Habari za kifo chake zimetangazwa na klabu ya St Duthus ya Tain, ambayo alikuwa meneja wake miaka ya 1990.

Wigan Athletic wamesema wamehuzunishwa sana kusikia habari za kifo chake.

"Alijiunga nasi kwa msimu mmoja miaka ya 1969 wakati ambao hatukuwa tunacheza soka ya ligi, lakini anakumbukwa sana na waliomtazama akicheza," anasema.

Ross alizaliwa Inver na kujiunga na Ross County mwaka 1961 akiwa na miaka 15.

Alifunga bao lake la kwanza katika klabu hiyo msimu huo.

Alifunga mabao 44 msimu wa 1964-65, mwaka ambao aliweka rekodi ya kufunga hat-trick.

Ross akiichezea Peterborough United mwaka 1966
Mkongwe mwenye rekodi ya kufunga 'Hat-Trick' ya kasi katika soka afariki Mkongwe mwenye rekodi ya kufunga 'Hat-Trick' ya kasi katika soka afariki Reviewed by Zero Degree on 5/19/2017 08:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.