Loading...

Tuzo nyingine aliyoshinda Ng'olo Kante Uingereza kwa msimu huu

Kiungo staa wa Ufaransa anayeichezea Klabu ya Chelsea ya England N’Golo Kante ametwaa tuzo nyingine msimu huu mara hii ikiwa ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Waandishi wa Habari za Michezo, FWA.


N’golo Kante baada ya kutwaa tuzo ya FWA
Katika hafla iliyofanyika Landmark Hotel Kante alipigiwa kura kushinda tuzo hiyo akiwapiku mchezaji mwenzie wa Chelsea Eden Hazard na mchezaji wa Tottenham Dele Alli kwa zaidi ya 65% ya kura zote.

Kabla ya tuzo ya FWA tayari N’Golo Kante alitwaa tuzo ya PFA na sasa anakuwa mchezaji wa 20 kutwaa tuzo hizo mbili kwa mkupuo mmoja.

Mwenyekiti wa FWA Patrick Barclay (kushoto) akimkabidhi N’golo Kante tuzo ya FWA

Tuzo nyingine aliyoshinda Ng'olo Kante Uingereza kwa msimu huu Tuzo nyingine aliyoshinda Ng'olo Kante Uingereza kwa msimu huu Reviewed by Zero Degree on 5/19/2017 08:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.