Loading...

Muntari afungiwa mechi moja baada ya kudai kubaguliwa, wenzake wapanga kugoma

Kiungo wa kati wa Pescara, Sulley Muntari amepigwa marufuku ya mechi moja baada ya kulalamikia matamshi ya kibaguzi.

Alipewa kadi ya manjano baada ya kumuomba refa asimamishe mechi siku ya Jumapili dhidi ya Cagliari akisema kuwa alikuwa akibaguliwa kwa misingi ya rangi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ghana mweye umri wa miaka 32, kisha akaondoka uwanjani hatua iliyosababisha apewe kadi ya pili ya manjano.

Maafisa wamesema kuwa sio mashabiki wengi walioonesha ubaguzi hadi kuweza kuchukua hatua hiyo.

Kamati ya nidhamu ilikubaliana kuwa vitendo hivyo vilikuwa vibaya lakini sera zake haziruhusu hatua kuchukuliwa kwa kuwa ni chini ya mashabiki 10 waliohusika.

Sasa aliyekuwa mshambulijia wa Tottenham, Garth Crook anasema kwa kila mchezaji wa kiafrika anayeheshimiwa katika ligi ya Itaia, anatakiwa kugoma wikendi hii ijayo endapo kama Sulley Muntari hatafutiwa adhabu hiyo ya kutocheza mechi moja.
Muntari afungiwa mechi moja baada ya kudai kubaguliwa, wenzake wapanga kugoma Muntari afungiwa mechi moja baada ya kudai kubaguliwa, wenzake wapanga kugoma Reviewed by Zero Degree on 5/04/2017 12:06:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.