Loading...

Muntari amezishutumu FIFA na UEFA kwa ubaguzi wa rangi

Shirikisho la Kandanda duniani na lile la Ulaya FIFA na UEFA, yamelalamikiwa kwa pamoja kuwa hayako makini katika kupambana na masuala ya ubaguzi wa rangi michezoni.

Kiungo raia wa Ghana anayechezea timu ya Pescara ya Italia Sulley Muntari ametoa lawama hizo katika mahojiano yake na BBC, baada ya kukutwa na tukio la kubaguliwa washabiki alipokuwa uwanjani wakati wa michuano ya Ligi ya Italia inayojulikana kama Serie A.

Sulley Muntari amezishutumu FIFA na UEFA, kwamba wanajali kile tu ambacho wanakitaka, na kusema kuwa kama taasisi hizo zingetaka kupambana na ubaguzi zingekuwa za kwanza kuingilia kati suala lake.

Amesema badala yake ni Umoja wa Mataifa tu, ndio umefanya hivyo mara tu baada ya kuliona tukio hulo na kuchukua hatua mara moja.

Katika mahojiano yake hayo na BBC, amesema ubaguzi upo kila sehemu na kwamba hali inazidi kuwa mbaya zaidi na kwamba kunaumuhimu kwa wachezaji kuungana pamoja na kupaza sauti zao kupinga vitendo hivyo.

Aidha amezitaka nchi nyingine kufuata mfano wa Uingereza kutokana na kutokuwa na vitendo hivyo vya kibaguzi katika ligi kuu yake.

Hata hivyo Sulley Muntari ameweka matumaini yake kwa Rais Mpya wa FIFA Gianni Infantino kwamba atafanya kitu, kubadili hali hiyo kutokana na kwamba ana mawazo tofauti.
Muntari amezishutumu FIFA na UEFA kwa ubaguzi wa rangi Muntari amezishutumu FIFA na UEFA kwa ubaguzi wa rangi Reviewed by Zero Degree on 5/09/2017 07:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.