Mvua kubwa kuendelea kunyesha – Mamlaka ya Hali ya Hewa [TMA] imetoa tahadhari
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), imewatahadharisha watanzania kuwa wakati huu msimu wa mvua za masika ukielekea ukingoni, wananchi wanatakiwa kufuatilia taarifa zinazoendelea kutolewa ili kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazoweza kutokea.
Msimu wa mvua za masika ulianza Machi na unatarajiwa kuisha Mei mwaka huu, katika maeneo ya Ukanda wa Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Maeneo mengine ni Pwani ya Kaskazini katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a,amesema kuwa mvua hizo zimeendelea kupungua wakati zikifikia ukingoni.
Aliendelea kusema katika maeneo hayo na yale ya kuzunguuka Ziwa Victoria wanapata mvua mara mbili kwa mwaka ambazo ni mvua za vuli na masika na kwamba kwa mwaka huu zilikuwa kubwa.
Alisisitiza kuwa msimu wa mvua kubwa bado unaendelea, ingawa zinaelekea ukingoni.
Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a,amesema kuwa mvua hizo zimeendelea kupungua wakati zikifikia ukingoni.
“Mvua zinaendelea kupungua, lakini matukio machache ya mvua kubwa yanaweza kuwatokea, hivyo wananchi wanatakiwa kutufuatilia taarifa tunazotoa ili kuchukua tahadhari ingawa zimepungua lakini hatuwezi kusema zimeisha hadi msimu umalizike,” Alisema Dkt Chang’a
Aliendelea kusema katika maeneo hayo na yale ya kuzunguuka Ziwa Victoria wanapata mvua mara mbili kwa mwaka ambazo ni mvua za vuli na masika na kwamba kwa mwaka huu zilikuwa kubwa.
Alisisitiza kuwa msimu wa mvua kubwa bado unaendelea, ingawa zinaelekea ukingoni.
Mvua kubwa kuendelea kunyesha – Mamlaka ya Hali ya Hewa [TMA] imetoa tahadhari
Reviewed by Zero Degree
on
5/19/2017 07:23:00 PM
Rating: