Loading...

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha St. Joseph akutwa na bastola pamoja na risasi 13

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Lazaro Mbise (23) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kukutwa na bastola pamoja na risasi 13 ambayo alimwibia baba yake.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mwanafunzi huyo alipokamatwa alikiri kuiba bastola hiyo pamoja na fedha kiasi cha Sh800, 000.

“Bastola hiyo ni LUGER cz100, mtuhumiwa alikiri aliiba pamoja na risasi kutoka kwa baba yake,” amesema Sirro. 

Kamishna Sirro ameagiza mzazi wa mtuhumiwa kukamatwa ili afikishwe mahakamani kwa kosa la kutohifadhi bastola yake vizuri.
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha St. Joseph akutwa na bastola pamoja na risasi 13 Mwanafunzi wa chuo kikuu cha St. Joseph akutwa na bastola pamoja na risasi 13 Reviewed by Zero Degree on 5/10/2017 07:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.