Loading...

Maalim Seif atinga kanisani kwa Gwajima

LEO Mei 10, 2017, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hammad amekwenda kumtembelea Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, kanisani kwake Ubungo, Dar es Salaam.

Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya mazungumzo ya faragha na Maalim Seif, Askofu Gwajima amesema ujio wa kiongozi huyo kanisani hapo ulikuwa ni kwa ajili ya kubadilishana mambo mbalimbali kuhusu nchi na mahusiano yao.

“Maalim Seif ni rafiki yangu, ni siku nyingi tulikuwa hatujaonana, tumezungumzia mambo ya nchi mbalimbali na mahusiano yangu mimi na yeye.

“Unaweza kuwa na rafiki ambaye anafanya kazi tofauti na yako, anaweza kuwa daktari na wewe ukawa siyo daktari, hata serikali haikatazi urafiki.

“Nimemuuliza ni kipi kimempata Profesa (Lipumba) mpaka anavuruga chama chake, amenielezea ili na mimi nijue cha kufanya. (Akacheka).

“Mimi nilikuwa siufahamu sana mgogoro wao, lakini sasa hivi nimepata picha,” alisema Askofu Gwajima huku akiangua kicheko.
Maalim Seif atinga kanisani kwa Gwajima Maalim Seif atinga kanisani kwa Gwajima Reviewed by Zero Degree on 5/10/2017 08:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.