Loading...

Picha za aliyetekeleza shambulizi Manchester zawekwa hadharani


Picha za CCTV zinazomuonyesha Salman Abedi usiku aliofanya shambulizi katika ukumbi wa Manchester na kuwaua watu 22 zimetolewa.

Salman Abedi
Maeneo 14 yanasakwa na wanaume 11 wamekamtwa kwa kushukiwa kuhusika katika ugaidi.

Abedi alitambuliwa saa mbili baada ya shambulizi la siku ya Jumatatu.

Waziri mkuu Theresa May anasema kuwa kiwango cha tisho lililopo kimepunguzwa na wanajeshi waliotumwa kuwasaidia polisi wataondolewa kuanzia siku ya Jumatatu

Mamia ya polisi waliojihami wanaendelea kulinda mamia ya matamasha kote nchini Uingereza.

Mamia ya polisi walitumwa wakati mashabiki 50,000 walipohudhuria tamasha la 'Courteeners' kwenye uwanja wa kriketi wa Old Trafford, ambalo ni tamasha kubwa kufanyika mjini humo tangu shambulizi kutokea.

Ulinzi mkali uliwekwa Wembley
Ulinzi zaidi umewekwa leo wakati wa mbio za Great Manchester Run ambapo maelfu ya wanariadha wanatarajiwa kushiriki
Picha za aliyetekeleza shambulizi Manchester zawekwa hadharani Picha za aliyetekeleza shambulizi Manchester zawekwa hadharani Reviewed by Zero Degree on 5/28/2017 10:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.