Loading...

Serengeti boys kukipiga dhidi ya Mali leo jumatatu

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa Miaka 17, Serengeti Boys, leo Jumatatu inafungua pazia lake katika mashindano ya Kombe la Afrika kwa Vijana, kwa kumenyana na Mali katika michuano hiyo inayofanyika nchini Gabon.

Serengeti Boys ipo Kundi B, pamoja na timu nyingine za Angola na Niger ambazo nazo zitakuwa kibaruani leo.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Bakari Shime, alisema kuwa kikosi chake kipo vizuri na kimejiandaa vya kutosha kuwakabili vijana wa Mali kwenye mchezo huo wa kwanza.

“Kikosi kipo vizuri na tumejipanga kuikabili vilivyo timu ya Mali kwani tunataka kuwafurahisha Watanzania kwa kutowaangusha na naomba wazidi kutuombea,” alisema Bakari Shime.

Baada ya mchezo wa leo Jumatatu, Serengeti itakuwa kibaruani tena Alhamisi hii itakapovaana na Angola.
Serengeti boys kukipiga dhidi ya Mali leo jumatatu Serengeti boys kukipiga dhidi ya Mali leo jumatatu Reviewed by Zero Degree on 5/15/2017 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.