Loading...

Watu 5 wa familia moja walioangukiwa na mti Arusha wazikwa siku moja

MAZIKO ya watu watano wa familia moja waliofariki baada ya mti kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala usiku wiki iliyopita, yalifanyika kwa simanzi kubwa mwishoni mwa wiki.

Marehemu hao ni Jophrey Jonathan (31), Lazaro
Lomayani (26), Kathbet Jonathan (20), Jonathan (9) na Mirium Balozi.

Walizikwa juzi katika Kijiji cha Ngiresi, Kata ya Sokoni 2 wilayani Arumeru, na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Mvua kubwa iliyonyesha Jumanne iliyopita iliangusha mti mkubwa uliokua jirani na nyumba waliyokuwa wamalala watu hao ambao walikufa papo hapo.

Akizungumza katika ibada ya maziko, Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Gideon Kivuyo aliwataka wafiwa kujipa moyo na kuendelea kupendana.

Alisema mtu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi na hukatwa mara moja kama ua linapochanua.

"Sisi kama binadamu tusibaki kuwa na huzuni na masikitiko bali tuendelee kujipa moyo na kupendana maana wenzetu wamemaliza yao hapa duniani," alisema. 

Alisema dayosisi imehuzunika kwa usharika wao kupoteza watu wengi kwa pamoja, lakini aliwataka waumini hao kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Watu 5 wa familia moja walioangukiwa na mti Arusha wazikwa siku moja Watu 5 wa familia moja walioangukiwa na mti Arusha wazikwa siku moja Reviewed by Zero Degree on 5/15/2017 11:39:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.