Loading...

Serengeti Boys yajibebea pointi 3 mbele ya Angola kwa ushindi wa goli 2-1

Serengeti Boys imepata ushindi wa kwanza wa michuano ya Afcon chini na taratibu ni dalili za kuingia hatua ya nusu fainali ambayo ni tiketi ya kucheza Kombe la Dunia.

Serengeti imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Angola na kupata pointi nne.

Mechi ya kwanza, Serengeti ilianza kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Mali ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Katika mchezo wa leo, Serengeti Boys ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 6 tu kupitia kwa Kelvin Naftali aliyeunganisha krosi safi ya Yohana Mkomola.

Angola awalijitutumua na kusawazisha katika dakika ya 18 kupitia kwa Pedro Augustino lakini Serengeti wakakomaa nao na kufunga bao la pili katika dakika ya 69 kwa bao la Abdul Selemani.
Serengeti Boys yajibebea pointi 3 mbele ya Angola kwa ushindi wa goli 2-1 Serengeti Boys yajibebea pointi 3 mbele ya Angola kwa ushindi wa goli 2-1 Reviewed by Zero Degree on 5/18/2017 10:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.