Loading...

Siri ya Usajili wa kishindo uliofanywa na Singida United yafichuka

WAKATI wadau wengi wa soka wakijiuliza siri ya usajili wa kishindo kwa timu ya Singida United, wenyewe wameibuka na kusema kuwa lengo lao ni kuwa na wachezaji wanaotambua majukumu yao.

Singida United iliyopanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, tayari imesajili wachezaji wa kimataifa wanne ambao ni Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Tafadwaza Kutinyu ambao wote ni Wazimbambwe pamoja na Shafik Batambuze raia wa Uganda.

Mratibu Mkuu wa Singida, Festo Richard Sanga, amesema siri ya usajili huo ni kuhakikisha msimu ujao unafanya vema, ikiwa sambamba na kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza.

“Sisi malengo yetu ni kufanya vema msimu ujao ndio mana tunasajili nyota ambao wapo timu za Taifa ambao tuna imani wanaweza kutuletea mafanikio kwenye dhamira yetu ya kubeba ubingwa au kushika nafasi nne za juu msimu ujao,” alisema.

Alisema kwa sasa wamebakiwa na nafasi tatu za usajili wa wachezaji wa kigeni ambapo zitajazwa kufuatiwa mapendekezo ya mwalimu wao, Hans Pluijm ambaye ataanza rasmi kukisuka kikosi hicho msimu ujao.

“Nafasi hizo tatu pia zitajazwa na nyota wanaopata nafasi kwenye timu zao za Taifa hata kama tutawasajili wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara na hili tunalifanya pia hata kwa wachezaji wazawa sharti letu lazima wawe wanaitwa kuitumikia Taifa Stars,” alisema.
Siri ya Usajili wa kishindo uliofanywa na Singida United yafichuka Siri ya Usajili wa kishindo uliofanywa na Singida United yafichuka Reviewed by Zero Degree on 5/18/2017 12:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.