Loading...

Baada ya Zimbabwe, Singida United sasa yatua Rwanda

TIMU ya Singida United baada ya kupanda ligi kuu haitaki mchezo, baada ya kumaliza na wazimbambwe watatu Tafadzwa Kutinyu kutoka Chicken Inn, Elisha Muroiwa na Wisdom Mtasa wote kutoka Dynamos ya Zimbambwe sasa inadaiwa kufika Rwanda kwa ajili ya kumalizana na Danny Usengimana mshambuliaji hatari wa Polisi ya Rwanda.

Habari kutoka ndani zinadai kwamba, Singida United wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Amavubi ya Rwanda Danny Usengimana, Singida United wanafanya siri ila rafiki wa karibu wa Usengimana amesema mchezaji huyo amemalizana tayari na Singida United na amesaini mkataba wa miaka miwili.

Danny Usengimana ni mchezaji hatari, katika msimu uliopita alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Rwanda. Hii sio mara ya kwanza kwa wachezaji wa Amavubi kuja kucheza Tanzania, Haruna Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji kutoka Rwanda anayecheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
Baada ya Zimbabwe, Singida United sasa yatua Rwanda Baada ya Zimbabwe, Singida United sasa yatua Rwanda Reviewed by Zero Degree on 4/10/2017 10:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.