Loading...

Serengeti boys yakubali kichapo Cameroon

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys imeshindwa kutamba mbele ya vijana wa Cameroon baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 katika mchezo wa marudiano uliofanyika mjini Yaounde, Cameroon.

Hichi ni kisasi kwa Cameroon baada ya wao kufungwa katika mchezo wa awali na timu hiyo a Serengeti boys uliofanyika jijini Dar.

Katika Mchezo wa awali, Serengeti Boys ilishinda bao 1-0 ukiwa umehudhuriwa na gwiji wa soka Abeid Pelle.

Kwa sasa timu ya Serengeti Boys wapo nchini Cameroon ambako wameweka kambi wakijiandaa na fainali za vijana za Afrika ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Gabon mwezi huu.
Serengeti boys yakubali kichapo Cameroon Serengeti boys yakubali kichapo Cameroon Reviewed by Zero Degree on 5/04/2017 03:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.