Loading...

Simba SC yarejea kileleni baada ya kuifunga Stand United goli 2-1

Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara baina ya klabu ya Simba Sc dhidi ya klabu ya Stand United umemalizika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, kwa klabu ya Simba kuchomoza na ushindi wa magoli 2 kwa 1 dhidi ya Stand United.

Wafungaji wa magoli hayo kwa upande wa klabu ya Simba ni mchezaji Juma Luizio anayecheza kwa mkopo kutoka Zesco United ya Zambia, aliyefunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya winga Shiza Kichuya.

Juma Luizio tena akawainua vitini mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la pili na la ushindi dakika ya 35, kwa mara nyingine akimalizia kazi nzuri ya Kichuya.

Kipindi cha pili milango ilikuwa migumu kwa pande zote mbili na Simba ikafanikiwa kuvuna pointi tatu kwa ushindi wa 2-1 na kurejea kileleni wakati kwa upande wa stand united mfungaji wa goli alikuwa Suleiman Kassim ‘Selembe’ aliyefunga sekunde ya 58 dakika ya kwanza.

Wekundu wa Msimbazi wanafikiwa kuwa na pointi 65 baada ya ushindi wa leo wakiwa wamecheza mechi 29, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 62, ambao wanaweza kurudi kileleni kwa mabao zaidi, wakiifunga Mbeya City kesho Uwanja wa Taifa.
Simba SC yarejea kileleni baada ya kuifunga Stand United goli 2-1 Simba SC yarejea kileleni baada ya kuifunga Stand United goli 2-1 Reviewed by Zero Degree on 5/12/2017 11:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.