Loading...

TCRA imewatahadharisha watumiaji wa kompyuta kuhusu Kirusi kiitwacho 'WANNACRY'

Shambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani.

Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000 za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry' duniani.

Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi.
Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.

Programu hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola 300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.Siku nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.

Tahadhari Iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuhusu Kirusi hicho:
TCRA imewatahadharisha watumiaji wa kompyuta kuhusu Kirusi kiitwacho 'WANNACRY' TCRA imewatahadharisha watumiaji wa kompyuta kuhusu Kirusi kiitwacho 'WANNACRY' Reviewed by Zero Degree on 5/14/2017 11:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.