Loading...

Kauli ya Nsajigwa kuhusu Obrey Chirwa wa Yanga

NAHODHA wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema kuwa Obrey Chirwa ni bonge la straika na kwamba anaweza kuwa somo tosha kwa washambuliaji wa Tanzania, hasa wale wanaochipukia.

Nsajigwa alisema: “Jamaa amejiongeza anafanya mazoezi yake binafsi, hii ndio inatakiwa na atawasumbua sana msimu ujao kama atajirekebisha katika suala la nidhamu, lakini kwa upande wa mazoezi sina shaka naye.”

Alisema kuwa, kwa wachezaji wanaojielewa, Mzambia huyo anaweza kuwa bonge la somo na kwamba watakaofanikiwa kufuata nyayo zake, anaweza kuwa tishio katika michuano ya ndani ya kimataifa.

Chirwa amekuwa moto wa kuotea mbali katika kuzifumania nyavu za timu pinzani kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo imebainika kuwa siri ya mafanikio yake ni mazoezi makali ya ziada anayofanya katika fukwe za bahari.

Katika siku za hivi karibuni, nyota huyo ambaye alisajiliwa na Yanga katika kipindi cha dirisha dogo mwaka jana, akitokea Platinum FC ya Zimbabwe, amekuwa nguzo muhimu kwa timu hiyo katika upachikaji wa mabao.

Mpaka sasa, Chirwa amekwishaipachikia timu ya Yanga mabao 11 na kumfanya kushika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu na kuwa miongoni mwa nyota wanaowania tuzo ya kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora msimu huu.

Straika huyo ameonekana akifanya mazoezi makali kivyake akiwa mapumzikoni katika fukwe za Msasani Beach, Coco Beach na Gymkhana, jijini Dar es Salaam na ndio sababu inayodaiwa kumfanya aonekane 
kuwa bora kwa sasa ni.

Akizungumzia kiwango chake cha sasa, Chirwa alisema ameamua kufanya mazoezi binafsi ili kujiweka fiti zaidi na kusisitiza huo ni mwanzo, bado moto zaidi unakuja huko mbeleni.

“Napenda sana kufanya mazoezi yangu binafsi ya ziada, kwa maana baada ya kugundua nina mapungufu sehemu nikaamua kujiongeza kwa kufanya mazoezi yangu binafsi nje ya timu,” alisema Chirwa.
Kauli ya Nsajigwa kuhusu Obrey Chirwa wa Yanga Kauli ya Nsajigwa kuhusu Obrey Chirwa wa Yanga Reviewed by Zero Degree on 5/14/2017 11:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.