Loading...

VIDEO: Crystal Palace walivyoikatia Hull City tiketi ya kushuka daraja kwa kuichakaza goli 4-0

Hull City waliondolewa kutoka Ligi ya Premier wakiwa na mecchi moja ya kucheza kufuatia kipigo kikali walichopewa na Crystal Palace.

Kikosi hicho cha Marco Silva kilipigwa na mshutuko na bao la dakika mbili na sekunde 11 baada ya kuanza kwa mechi.

Andrea Ranocchia alishindwa kuondoa mpira eneo la hatari, hali iliyompa fusra Wilfried Zaha kutizikisa nyavu za Hull City.

Bao la pili la Christian Benteke lilitimiza mabao mawili ya Crstal Palace huku mabao mengine mawili yakifungwa na Luka Milivojevic, na Patrick van Aanholt.

Hull City sasa wanaungana na Sunderland pamoja na Middlesbrough kusubiri msimu unaokuja.
VIDEO: Crystal Palace walivyoikatia Hull City tiketi ya kushuka daraja kwa kuichakaza goli 4-0 VIDEO: Crystal Palace walivyoikatia Hull City tiketi ya kushuka daraja kwa kuichakaza goli 4-0 Reviewed by Zero Degree on 5/15/2017 12:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.