Loading...

TANZIA: Aliyekuwa RC Ruvuma na aliyekuwa mwandishi wa habari wa Nyerere wamefariki leo

Aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Paul Sozigwa amefariki saa 8:30 usiku wa kuamkia leo.

Msemaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda amesema kuwa Sozigwa alikuwa anaendelea vizuri lakini akafariki wakati akiendelea na matibabu hayo.

Amesema alikuwa akiendelea na matibabu wodi namba mbili baada ya kutolewa kwenye wodi ya uangalizi maalumu.

"Ni kweli amefariki usiku wa kuamkia leo wodi namba mbili hapa JKCI." amesema Nkinda.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu
Kifo kingine ni cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amefariki dunia leo saa nne asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Mdogo wa marehemu, Shaibu Mwambungu amesema kaka yake alifariki dunia leo asubuhi baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa hospitalini hapo.

Shaib amesema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye ambapo kwa sasa anajiandaa kusafiri kutoka Songea kuja jijini Dar es salam kwa ajili ya mazishi.


TANZIA: Aliyekuwa RC Ruvuma na aliyekuwa mwandishi wa habari wa Nyerere wamefariki leo TANZIA: Aliyekuwa RC Ruvuma na aliyekuwa mwandishi wa habari wa Nyerere wamefariki leo Reviewed by Zero Degree on 5/12/2017 11:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.