Loading...

Zaidi ya bilioni 1 zatengwa kwa ajili ya mishahara Singida United

SINGIDA United wameonyesha kupania kikweli kweli msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya uongozi wa timu hiyo kutenga dau la Sh bilioni 1.6 kwa ajili ya mishahara ya wachezaji kwa mwaka.

Timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu, iko kwenye harakati za kuboresha kikosi chao pamoja na maandalizi mengine ya timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Singida, Festo Sanga, alisema wamejipanga kila idara katika kuhakikisha wanaingia kwa nguvu zote kwenye ligi hiyo.

Katika moja ya mikakati yao ni kuboresha mishahara ya wachezaji, ambapo watalipa Sh bilioni 1.6 pamoja na mahitaji mengine kama makazi na bima za afya.

“Singida tunajipanga kuhakikisha tunaingia Ligi Kuu kwa nguvu. Lengo kubwa likiwa ni kucheza michuano ya kimataifa na ili kufanikisha hilo lazima tuchukue ubingwa,” alisema Sanga.

“Hivyo kama uongozi tumejipanga kila idara, kulipa mishahara mizuri wachezaji wetu, nyumba za kuishi pamoja na bima za afya.”

Sanga aliongeza kwamba kwa sasa kocha wao Hans van Pluijm, bado anafuatilia wachezaji mbalimbali ili kuendelea kukisuka kikosi hicho kabla ya kuanza maandalizi ya msimu ujao.
Zaidi ya bilioni 1 zatengwa kwa ajili ya mishahara Singida United Zaidi ya bilioni 1 zatengwa kwa ajili ya mishahara Singida United Reviewed by Zero Degree on 5/09/2017 11:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.