Loading...

ACT-Wazalendo yamkana aliyejitangaza kurejea CCM mbele ya Rais Magufuli


Chama cha ACT-Wazalendo kimemkana Isihaka Karanda aliyetangazwa kwenye mkutano wa Rais John Magufuli kuwa ni Mwenyekiti wa ACT mkoa wa Pwani aliyeamua kurejea CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo (Alhamisi) Mwenyekiti wa ACT Mkoa wa Pwani, Mrisho Swagara amesema amesikitishwa na kitendo hicho, kwa kuwa CCM wameamua kumdanganya Rais Magufuli.

"Karanda alikuwa ni mwanachama wetu wa kawaida, lakini ni dhaifu hivyo siyo tegemeo, hii ni hatari kubwa Rais kupelekewa mtu asiye sahihi inaweza kuzua mambo tofauti," amesema. 

Swagara amesisitiza kuwa ACT imelichukulia jambo hili kuwa ni propaganda za CCM dhidi yao, kwa lengo la kuwahadaa wananchi.

Juzi, Jumanne, Karanda alitangaza kuhama ACT-Wazalendo na kuhamia CCM, mbele ya mkutamo wa hadhara wa Rais Magufuli katka viwanja vya Bwawani, Kibaha Mailimoja.

Alitangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole.

Source: Mwananchi
ACT-Wazalendo yamkana aliyejitangaza kurejea CCM mbele ya Rais Magufuli ACT-Wazalendo yamkana aliyejitangaza kurejea CCM mbele ya Rais Magufuli Reviewed by Zero Degree on 6/22/2017 02:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.