Loading...

Mashabiki wa Yanga wachukua uamuzi wa kuchoma moto jezi ya Haruna Niyonzima

Mashabiki wa Yanga wameonyesha hasira zao kwa kuchoma moto jezi ya Haruna Niyonzima.


Mashabiki hao wa Yanga wameonyesha kuchukizwa na uamuzi wa Niyonzima kutosaini mkataba Yanga baada ya kushindwana na uongozi wa klabu hiyo.


Jana mchana, uongozi wa Yanga kupitia katibu wake mkuu, Charles Boniface Mkwasa ulitangaza kumuacha Niyonzima kwenda anakohitaji baada ya mkataba wake kwisha.

Yanga imesisitiza, imempa Niyonzima mkono wa kheri kwa kuwa haina uwezo wa kumsajiri tena.

Mashabiki hao wanaoelezwa kuwa ni wa Dar es Salaam, wamesikika wakipongezana kutokana na uamuzi wao wa kuchoma jezi hiyo namba 8 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Niyonzima aliyeichezea Yanga kwa miaka sita.
Mashabiki wa Yanga wachukua uamuzi wa kuchoma moto jezi ya Haruna Niyonzima Mashabiki wa Yanga wachukua uamuzi wa kuchoma moto jezi ya Haruna Niyonzima Reviewed by Zero Degree on 6/22/2017 09:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.