Loading...

Rasmi Yanga SC yathibitisha kuachana na Haruna Niyonzima


Baada ya tetesi za muda mrefu kuwa mchezaji wa Yanga na timu ya taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima kuwa ameachana na timu yake ya Yanga, uongozi wa klabu ya Yanga umetoa taarifa kuhusu mchezaji huyo, isome hapa chini.

TAARIFA KWA UMMA:

Klabu ya Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu.

Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.

Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla.

Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo
Young Africans Sports club.
21-06-2017.
Rasmi Yanga SC yathibitisha kuachana na Haruna Niyonzima Rasmi Yanga SC yathibitisha kuachana na Haruna Niyonzima Reviewed by Zero Degree on 6/21/2017 03:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.