Loading...

Rais Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Dawasa kuachia ngazi


Rais John Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Archado Mtalemwa ajiandae kustaafu kutokana na mapungufu mengi ambayo Rais amesema ameyaona katika mamlaka hiyo.

Rais ameyasema hayo leo(Jumatano) akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani na alitumia fursa hiyo kuzungumzia miradi ya maji na ulipaji wa maji kwa taasisi za serikali.

“Ndugu yangu Mtalemwa, naongea kwa lugha nzuri hapa, nikuombe tu kuwa ustaafu mapema, inawezekana Waziri wa Maji ni rafiki yako, kama ilivyo kwa mawaziri wengine, lakini nadhani huu ni wakati mzuri,” amesema na kuongeza;

“Pamoja na kazi zako nzuri, it’s your time to go.”

Amezungumzia kero mbalimbali za maji na kusema kuna upotevu mkubwa wa maji.

Rais amemuagiza Waziri wa Maji, Gerson Lwenge kuhakikisha mradi wa maji wa Ng’apa- Lindi, unakamilika haraka, ikiwezekana waziri ahamie hukohuko.
Rais Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Dawasa kuachia ngazi Rais Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Dawasa kuachia ngazi Reviewed by Zero Degree on 6/21/2017 08:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.