Bodaboda watajwa kuwa vinara wa unyanyasaji wa kimapenzi kwa wasichana
Kwa mujibu wa matokeo ya Utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la Maadili Center na kutolewa jana na Mwenyekiti wa shirika hilo, Florentine Senya, watoto wengi wa kike walitaja kero kubwa kuwa, waendesha pikipiki hao (bodaboda) huwanyanyasa hadi kufikia hatua ya kutishia kuwagonga kwa pikipiki zao wasichana hao wanapokataa kujihusisha nao kimapenzi.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utafiti wa malezi na maadili ya watoto wa kike uliofanywa na shirika hilo, Senya amesema utafiti huo unaoendelea hadi sasa ulifanywa katika shule za sekondari na msingi kwa mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, utafiti huo pia umebaini kuwa asilimia 78 ya familia nyingi zina matatizo ikiwemo wazazi kutelekeza familia zao na kuwaacha wengi kujihudumia wenyewe jambo linalochangia kuwapo ongezeko la watoto wasio na maadili.
Senya ameongeza kwa kusema kuwa utafiti umebaini watoto wa kike 10 kati ya 50 sawa na asilimia 20, wamepitia vitendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo kupigwa na wazazi, kuchomwa moto wanapokosea, na hata kutishiwa maisha wanapokataa kujihusisha kimapenzi na watu waliowazidi umri.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Maadili Center, Bi. Rosaline Castillo alitaka jamii ikubali ukweli kuwa wazazi wengi wametelekeza watoto katika malezi.

Reviewed by Zero Degree
on
6/29/2017 04:54:00 PM
Rating: